Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 5 October 2016

Rais Magufuli afanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja ndege DSM upande wa Terminal One

#UGANDA:Baba akamatwa kwa kumzika mwanaye wa kiume( 5) katika kichuguu akiwa hai kwa madai ya kumuepusha na vitisho vya mama yake wa kambo

Goodluck Gozbert afunguka kuhusu mahusiano yake Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa nchini, Goodluck Gozbert akanusha kuonekana akijivinjari na mwanamke yeyote kwa sasa na kusema muda ukifika wa yeye kuwa kwenye mahusiano basi atakuwa. Akiongea na eNewz, Gozbert alijibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na uvumi wa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akionekana na mwanamke wakijiachia naye na kudaiwa kuwa ndiye mpenzi wake ambapo alikanusha. “Sina mwanamke kwa sasa na maneno ya watu yasikuchanganye, Ikifikia wakati wa Mungu kwa mimi kuwa kwenye mahusiano basi nitakuwa kwenye mahusiano ya ndoa” alisema Gozbert. Hata hivyo Goodluck aliendelea kusema kuhusiana na muziki wa injili kuwa ni aina ya muziki ambao hauhitaji kiki kwa hiyo siku atakapokuwa tayari kwa swala la ndoa ataweka wazi kwa jamii inayomzunguka.

Wadau wa uvuvi wajadili changamoto ya usalama Ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kazi katika sekta ya uvuvi imekuwa ni suala linalogonga vichwa vya habari.Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, kazi za shuruti, usafirishaji haramu wa watu, ajira kwa watoto, usalama mdogo katika vyombo vya uvuvi na kwenye viwanda vya samaki ni masuala ambayo yamekuwa yakiarifiwa kote duniani. Hali hii imezifanya serikali na wadau katika sekta ya uvuvi kutoa kipaumbele cha kutaka kupata suluhu ya matatizo hayo. Wawakilishi kutoka sekta ya uvuvi, asasi za kiraia, zikiwemo jumuiya za wavuvi, wawakilishi wa serikali na mashirika ya kimataifa ikiwemo FAO wanakutana mjini Vigo Hispania ili kujadili na kupata suluhu. Afisa wa uvuvi katika shirika la FAO Uwe Barg amesema kuna ukosefu wa ajira za kutosha, pia fursa za ajira kwa wanawake na vijana ambazo hazitumiki, lakini pia tatizo la usalama wa kijamii ikiwemo likizo ya uzazi, malipo ya uzeeni, kima cha chini cha malipo na kunahitajika mjadala jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi.

Monday, 3 October 2016

Zimebaki siku 10, zoezi la kuchukua fomu na kurudisha kukamilika

Wafanyabiashara wa Soko la Morogoro wamekubali kubomoa na kuhamishia mizigo yao sehemu nyingine ili kupisha ujenzi wa soko jipya baada ya mvutano uliodumu kwa muda wa miaka miwili.Soko Kuu la Morogoro nyakati za Mvua. Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imesema kuwa kukataa kwa wafanyabiashara hao kulikuwa kunaisababishia halmashauri ya Manispaa ya Morogoro hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4 Kwa sasa wafanyabiashara hao wamehamishia biashara zao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi kwa muda katika soko la Manzese na Nane-Nane Mkoani humo. Aidha wafanyabiashara hao wameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili likamilike kwa muda muafaka ambapo ni kipindi cha mwaka mmoja kama ilivyopangwa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Kulwa Mgalula amesema kuwa Halmashauri itazingatia mikataba iliyopo kati yake na wafanyabiashaara hao katika kuwarejesha.

Wafanyakazi wa Sekta ya Sukari nchini Kenya wametaka kuwepo kwa uwazi pamoja na mashauriano mapana kuhusiana na uagizaji sukari kutoka nje.Kauli hiyo inakuja wakati huu ambapo Wizara ya Kilimo Kenya ikiendelea kutoa vibali vya uagizaji sukari nje, ili kukabiliana na upungufu. Nchi ya Kenya kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa kila mwaka wa upatikanaji wa sukari, ambao unakadiriwa kufikia sukari tani laki mbili hadi laki mbili na nusu kwa mwaka. Mamlaka inayohusika na uratibu wa sukari nchini Kenya imetoa vibali vya uagizaji sukari tani elfu 9 kwa mwezi Agosti na tani elfu 15 za sukari katika mwezi Septemba. Katibu wa Chama cha Wakulima wa Miwa Kenya na wafanyakazi wa sekta hiyo Bw. Francis Wangara amemsihi mratibu wa sekta hiyo kufuata taratibu zinazostahili katika uagizaji wa sukari kutoka nje, kwa kuhakikisha uwazi na ushirikishwaji wa wadau wenye viwanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Prof. Lawrence Mujungu Museru Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016. Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.