Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 5 October 2016

Wadau wa uvuvi wajadili changamoto ya usalama Ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kazi katika sekta ya uvuvi imekuwa ni suala linalogonga vichwa vya habari.Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, kazi za shuruti, usafirishaji haramu wa watu, ajira kwa watoto, usalama mdogo katika vyombo vya uvuvi na kwenye viwanda vya samaki ni masuala ambayo yamekuwa yakiarifiwa kote duniani. Hali hii imezifanya serikali na wadau katika sekta ya uvuvi kutoa kipaumbele cha kutaka kupata suluhu ya matatizo hayo. Wawakilishi kutoka sekta ya uvuvi, asasi za kiraia, zikiwemo jumuiya za wavuvi, wawakilishi wa serikali na mashirika ya kimataifa ikiwemo FAO wanakutana mjini Vigo Hispania ili kujadili na kupata suluhu. Afisa wa uvuvi katika shirika la FAO Uwe Barg amesema kuna ukosefu wa ajira za kutosha, pia fursa za ajira kwa wanawake na vijana ambazo hazitumiki, lakini pia tatizo la usalama wa kijamii ikiwemo likizo ya uzazi, malipo ya uzeeni, kima cha chini cha malipo na kunahitajika mjadala jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment