Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, 3 October 2016

Wafanyabiashara wa Soko la Morogoro wamekubali kubomoa na kuhamishia mizigo yao sehemu nyingine ili kupisha ujenzi wa soko jipya baada ya mvutano uliodumu kwa muda wa miaka miwili.Soko Kuu la Morogoro nyakati za Mvua. Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imesema kuwa kukataa kwa wafanyabiashara hao kulikuwa kunaisababishia halmashauri ya Manispaa ya Morogoro hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4 Kwa sasa wafanyabiashara hao wamehamishia biashara zao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi kwa muda katika soko la Manzese na Nane-Nane Mkoani humo. Aidha wafanyabiashara hao wameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili likamilike kwa muda muafaka ambapo ni kipindi cha mwaka mmoja kama ilivyopangwa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Kulwa Mgalula amesema kuwa Halmashauri itazingatia mikataba iliyopo kati yake na wafanyabiashaara hao katika kuwarejesha.

No comments:

Post a Comment