Thursday, 22 September 2016
Msanii Barnaba Classic ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa 'lover boy, ametoa sababu inayomfanya asiihusishe sana familia yake kwenye maisha yake ya sanaa, na kusema siyo kitu anachokipa kipaumbele.Barnaba Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Baranaba amesema yeye kama baba wa familia anaijali sana familia yake, na hataki aihusishe na maisha ya sanaa, isispokuwa mashabiki wanachotakiwa kujua ni kazi zake za sanaa tu. "Mimi napenda sana familia yangu, lakini sidhani kama inahitajika kuleta mahusiano yako au familia yako mbele ya hadhara au ya jamii ambayo unaifanyia kazi, sidhani kama maisha yangu ya muziki yanalingana na maisha yangu ya nyumbani, lakini huenda yakawa kichocheo katika sanaa yangu, lakini si kitu ambacho naweza kikawa serious ikawa muda wote watu wanione, hapana" alisema Baranaba. Barnaba aliendelea kwa kusema..... "lakini pia mi ni mtu ambaye nina familia ambayo naitazama tofauti, naipenda familia yangu, napenda wakae kwenye mazingira kama familia, nikirudi nyumbani niwe Elias, nikitoka nje na kwenye kazi yangu naitwa Barnaba, naweka mbali kidogo kumleta mtoto wangu haya mambo, na nina mipango mingi sana na familia yangu lakini sidhani kama jamii inatakiwa ijue zaidi, wao wanachotakiwa wajue ni sanaa yangu na muziki wangu unakwendaje", alisema Barnaba. Barnaba amekuwa mtu wa kuepuka habari za skendo tangu amekuwa baba wa familia, kitu ambacho wasanii wengi hushindwa kuhimili kutenganisha maisha yao ya muziki na maisha binafsi ya familia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment