Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 21 September 2016

Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 17 inatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kambi ya siku 10 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville.Mchezo huo utakaopigwa Oktoba 02 ni wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana zitakazofanyika nchini Madagascar mwaka 2017. Kocha wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime amesema, wanaamini mchezo wa marudiano utakuwa na changamoto nyingi lakini wanaamini watajitahidi ili kuhakikisha wanashinda na kuweza kushiriki AFCON hapo mwakani. Shime amesema, anaamini Serikali ya Tanzania ina mkono mrefu hivyo ameiomba kuendelea kutoa sapoti hata timu hiyo itakapokuwa nchini Congo Brazzaville kwa ajili ya mchezo huo ili kuiweka timu ya Serengeti Boys katika hali ya usalama zaidi na kujiona hawapo ugenini. Kwa upande mwingine Shime amewataka watanzania kutokuwa na wasiwasi na timu yao kwani wamejiandaa kushinda kila wakati na wanajitahidi ili kuweza kupata matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano ambayo yatawaweka katika nafasi nzuri.

No comments:

Post a Comment