Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, 21 September 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema, hivi sasa wanaendelea na jitihada za kukuza mchezo wa mpira wa magongo nchini.Miongoni mwa mikakati ni pamoja na kushirikiana na Rais wa chama cha mchezo huo duniani FIH pamoja na Rais wa chama cha mchezo huo barani Afrika AFHA ambao wapo nchini kwa ajili ya mikakati ya kuboresha miundombinu na kurudisha heshima ya mchezo huo kama zamani. Nape amesema, mpira wa Magongo (Hockey) ni mchezo ambao ulileta heshima kubwa sana kwa nchi miaka ya nyuma lakini kwa sasa umekuwa haufanyi vizuri katika mshindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi hivyo anaamini ushirikiano huo utasaidia kurudisha hadhi ya mchezo huo nchini. Nape amesema, ameshaongea na Rais wa FIH Leandro Nerge na ameahidi Uwanja ambao utakuwa ukitumika kwa ajili ya mchezo huo na amekiagiza chama cha mchezo wa mpira wa Magongo nchini THA kuandika barua kwa wizara ya michezo ili waweze kuwasiliana na Wizara ya Ardhi ili kuweza kupata eneo zuri litakalojengwa Uwanja. Nape amesema, kwa upande wa Rais wa AFHF Seif Ahmed ameahidi kuongeza miundombinu ya uwanja ikiwa ni pamoja na taa za uwanjani ili kuufanya uwanja kuwa bora zaidi katika matumizi ya mashindano mbalimbali Wakati huohuo Waziri Nape Nnauye ametoa pongezi kwa timu ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens mara baada ya jana kutawazwa kuwa mabingwa wa kwanza kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na kati. Waziri Nape amesema, wameanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu na wataendelea kutoa sapoti kwa timu hiyo ili iweze kuiwakilisha nchi vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment