Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, 22 September 2016

Ripoti ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu mkoani Morogoro na kuundiwa tume ya uchunguzi hivi karibuni, leo imekabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Waziri Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara mkoani Morogoro kushuhudia athari za mapigano ya mgogoro wa ardhi uliosababisha mifugo kadhaa kuuawa kwa kukatwa mapanga. Mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 Mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani ambavyo husababisha vifo vya watu na mifugo huenda ukatatuliwa kikamilifu baada ya kuwasilishwa kwa mapendekeo ya Tume ya Jaji Jacob Mwambegele wa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania. Akipokea ripoti ya mapendekezo hayo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Luvuki, amesema kwa muda mrefu serikali ilishindwa kutua mgogoro huo hivyo ripoti hiyo itakuwa mwanzo wa utatuzi wa mgogoro huo kwani wametumia chombo huru ambacho ni Mahakama katika kuamua namna ya kutatua mgogoro huo. Hatua ya serikali kutumia Mahakama ni ya kwanza kuwahi kutokea, Jambo ambalo Mhe. Lukuvi amesema linatoa fursa ya tume hiyo kutoingiliwa na upande wowote unaohusishwa katika mgogoro huo na kwamba anakiri mapungufu yote yaliyoainishwa kwenye ripoti hiyo inayohusu Wizara yake. Aidha, ripoti hiyo yenye mapendekezo makuu 6 inayohusisha mogogoro wa ardhi mkoani Morogoro katika vijiji vya Mabwegere itawasilishwa kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa kwa wizara zote zinazohusishwa ikiwemo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Vijini hivyo ni Dumila, Madegwa, Mabwegere na Matongolo vyote vya Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ambavyo vimekumbwa na mauaji ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kwa zaidi ya miaka 20.

No comments:

Post a Comment