Monday, 17 October 2016
Thursday, 6 October 2016
Wednesday, 5 October 2016
Goodluck Gozbert afunguka kuhusu mahusiano yake Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa nchini, Goodluck Gozbert akanusha kuonekana akijivinjari na mwanamke yeyote kwa sasa na kusema muda ukifika wa yeye kuwa kwenye mahusiano basi atakuwa. Akiongea na eNewz, Gozbert alijibu hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na uvumi wa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akionekana na mwanamke wakijiachia naye na kudaiwa kuwa ndiye mpenzi wake ambapo alikanusha. “Sina mwanamke kwa sasa na maneno ya watu yasikuchanganye, Ikifikia wakati wa Mungu kwa mimi kuwa kwenye mahusiano basi nitakuwa kwenye mahusiano ya ndoa” alisema Gozbert. Hata hivyo Goodluck aliendelea kusema kuhusiana na muziki wa injili kuwa ni aina ya muziki ambao hauhitaji kiki kwa hiyo siku atakapokuwa tayari kwa swala la ndoa ataweka wazi kwa jamii inayomzunguka.
Wadau wa uvuvi wajadili changamoto ya usalama Ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kazi katika sekta ya uvuvi imekuwa ni suala linalogonga vichwa vya habari.Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, kazi za shuruti, usafirishaji haramu wa watu, ajira kwa watoto, usalama mdogo katika vyombo vya uvuvi na kwenye viwanda vya samaki ni masuala ambayo yamekuwa yakiarifiwa kote duniani. Hali hii imezifanya serikali na wadau katika sekta ya uvuvi kutoa kipaumbele cha kutaka kupata suluhu ya matatizo hayo. Wawakilishi kutoka sekta ya uvuvi, asasi za kiraia, zikiwemo jumuiya za wavuvi, wawakilishi wa serikali na mashirika ya kimataifa ikiwemo FAO wanakutana mjini Vigo Hispania ili kujadili na kupata suluhu. Afisa wa uvuvi katika shirika la FAO Uwe Barg amesema kuna ukosefu wa ajira za kutosha, pia fursa za ajira kwa wanawake na vijana ambazo hazitumiki, lakini pia tatizo la usalama wa kijamii ikiwemo likizo ya uzazi, malipo ya uzeeni, kima cha chini cha malipo na kunahitajika mjadala jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi.
Monday, 3 October 2016
Wafanyabiashara wa Soko la Morogoro wamekubali kubomoa na kuhamishia mizigo yao sehemu nyingine ili kupisha ujenzi wa soko jipya baada ya mvutano uliodumu kwa muda wa miaka miwili.Soko Kuu la Morogoro nyakati za Mvua. Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imesema kuwa kukataa kwa wafanyabiashara hao kulikuwa kunaisababishia halmashauri ya Manispaa ya Morogoro hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4 Kwa sasa wafanyabiashara hao wamehamishia biashara zao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi kwa muda katika soko la Manzese na Nane-Nane Mkoani humo. Aidha wafanyabiashara hao wameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili likamilike kwa muda muafaka ambapo ni kipindi cha mwaka mmoja kama ilivyopangwa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Kulwa Mgalula amesema kuwa Halmashauri itazingatia mikataba iliyopo kati yake na wafanyabiashaara hao katika kuwarejesha.
Wafanyakazi wa Sekta ya Sukari nchini Kenya wametaka kuwepo kwa uwazi pamoja na mashauriano mapana kuhusiana na uagizaji sukari kutoka nje.Kauli hiyo inakuja wakati huu ambapo Wizara ya Kilimo Kenya ikiendelea kutoa vibali vya uagizaji sukari nje, ili kukabiliana na upungufu. Nchi ya Kenya kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa kila mwaka wa upatikanaji wa sukari, ambao unakadiriwa kufikia sukari tani laki mbili hadi laki mbili na nusu kwa mwaka. Mamlaka inayohusika na uratibu wa sukari nchini Kenya imetoa vibali vya uagizaji sukari tani elfu 9 kwa mwezi Agosti na tani elfu 15 za sukari katika mwezi Septemba. Katibu wa Chama cha Wakulima wa Miwa Kenya na wafanyakazi wa sekta hiyo Bw. Francis Wangara amemsihi mratibu wa sekta hiyo kufuata taratibu zinazostahili katika uagizaji wa sukari kutoka nje, kwa kuhakikisha uwazi na ushirikishwaji wa wadau wenye viwanda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Prof. Lawrence Mujungu Museru Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016. Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Saturday, 24 September 2016
Pambano la Tyson Fury na Klitschko layeyukaBingwa wa masumbwi ya uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha pambano lake na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwa sababu ya afya yake kuwa katika hatihati.Wladimir Klitschko na Tyson Fury Ingawa mapromota wa bondia huyo hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema "Hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo la maruduiano". Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana. Pambano la marudiano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunjika fupa la kisigino chake huku Pambano jipya la marejeo lilipangwa kufanyika Oktoba 29.
Makorokocho waibuka mabingwa Dance100% 2016 Shindano la Dance100% 2016 limemalizika leo katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam ambapo kundi la Makorokocho limeibuka na ubingwa na kujipatia kitita cha milioni 7, Kombe la Dance100% pamoja na cheti maalum.Ushindi wa Team Makorokocho umekuja baada ya makundi yote 6 kucheza raundi ambapo raundi ya kwanza Mega Mix waliyoandaliwa, na ilichezwa na makundi yote ikiwa na jumla ya alama 60% huku raundi ya pili ikiwa na alama 40% ambapo kila kundi lilijichagulia wimbo wake wa kucheza. . Baada ya kazi ya raundi zote mbili kazi ya majaji ilikamilishwa na shughuli ya kumuisha matokeo na hatimaye kundi la Team Makorokochokuibuka na ushindi mwaka huu kutokana na uwezo waliouonesha katika raundi zote mbili na kuyapiku makundi yote. Akizungumza baada ya kuibuka washindi wa shindano hilo Hamadi Abasi amesema umoja na mshikamano katika kundi lao ndicho chanzo kikuu cha wao kuweza kuibuka na ushindi wa shindano hilo. “Sisi kutokana na umoja wetu tumekuwa zaidi ya ndugu ndiyo maana tumeweza kuwa wamoja katika mazoezi na kujituma na kuangalia wenzetu wana upungufu gani tukaufanyia kazi na hatimaye tukatangazwa washindi” Amesema Hamadi. Hamadi ameongeza kuwa ushindi wao hauna ubishi wowote kwa kuwa ukiondoa majaji pia hadhira ambayo imeshiriki kutizama shindano wameona kazi ambayo wameoinesha . Matokeo yote kwa makundi yote 6 yaliyoshiriki fainali ni kama ifuatavyo kwa mpangilio wa namba. Timu Makorokocho J Combat D.D.I Crew Clever Boys Wazawa Crew na kundi la mwisho ni B.B.K Boys Baadhi ya mashabiki ambao wameongea na EATV wamesema kundi hilo linastahili ushindi huo kutokana na namna ambavyo kuanzia mwanzo wa shindano hilo wameonesha dhamira ya kutaka ushindi kwa kuwa wabunifu kila siku wanaposhiriki shindano. Shindano la Dance100% ambalo limefikia tamati leo litaoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni chini ya udhamini wa Vodacom pamoja na Coca – Cola.
Thursday, 22 September 2016
Kocha Jose Mourinho wa Man United, kwa mara nyingine tena atalazimika kukutana uso kwa uso na mbabe wake Pep Guadiola wa Man City, katika mchezo wa raundi ya 4 ya michuano ya Kombe la ligi nchini England, lijulikanalo kama EFL Cup kwa msimu huu.Jose Mourinho akimpongeza Pep Guadiola Kwa mujibu wa droo iliyotolewa usiku wa kuamkia leo mara baada ya kumalizika kwa michezo ya raundi tatu, Mancheste United imepangwa kukutana na Manchester City katika dimba la Old Trafford, wiki inayoaanzia Oktoba 24 mwaka huu. Man United imefikia hatua hiyo baada ya kuichapa Northampton mabao 3-1, huku Manchester City ikipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea City. Mechi hiyo itakuwa ni ya kulipiza kisasi au kuendeleza ubabe, baada ya wawili hao kukutana kwa mara ya kwanza katika ligi ya England, Septemba 10, mwaka huu na City kupata ushindi wa 2-1. Droo hiyo pia imewagonganisha wakali wengine wa soka la England, ambao ni Liverpool itakayokabana koo na Tottenham katika dimba la Anfield, huku West Ham wakipangwa kuchujana na Chelsea. Kwa upande wao Arsenal, huenda wakawa na kazi rahisi mbele ya Reading. Matokeo kamili ya droo hiyo yapo kama ifuatavyo. West Ham v Chelsea Manchester United v Manchester City Arsenal v Reading Liverpool v Tottenham Bristol City v Hull Leeds v Norwich Newcastle v Preston Southampton v Sunderlan
Ripoti ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu mkoani Morogoro na kuundiwa tume ya uchunguzi hivi karibuni, leo imekabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Waziri Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara mkoani Morogoro kushuhudia athari za mapigano ya mgogoro wa ardhi uliosababisha mifugo kadhaa kuuawa kwa kukatwa mapanga. Mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 Mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani ambavyo husababisha vifo vya watu na mifugo huenda ukatatuliwa kikamilifu baada ya kuwasilishwa kwa mapendekeo ya Tume ya Jaji Jacob Mwambegele wa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania. Akipokea ripoti ya mapendekezo hayo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Luvuki, amesema kwa muda mrefu serikali ilishindwa kutua mgogoro huo hivyo ripoti hiyo itakuwa mwanzo wa utatuzi wa mgogoro huo kwani wametumia chombo huru ambacho ni Mahakama katika kuamua namna ya kutatua mgogoro huo. Hatua ya serikali kutumia Mahakama ni ya kwanza kuwahi kutokea, Jambo ambalo Mhe. Lukuvi amesema linatoa fursa ya tume hiyo kutoingiliwa na upande wowote unaohusishwa katika mgogoro huo na kwamba anakiri mapungufu yote yaliyoainishwa kwenye ripoti hiyo inayohusu Wizara yake. Aidha, ripoti hiyo yenye mapendekezo makuu 6 inayohusisha mogogoro wa ardhi mkoani Morogoro katika vijiji vya Mabwegere itawasilishwa kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa kwa wizara zote zinazohusishwa ikiwemo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Vijini hivyo ni Dumila, Madegwa, Mabwegere na Matongolo vyote vya Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ambavyo vimekumbwa na mauaji ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kwa zaidi ya miaka 20.
Kocha wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique, amesema kikosi chake kitabaki imara ingawa kitamsubiria Lionel Messi aliyepatwa majeruhi kwenye mchezo wa jana wa sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.Lionel Messi Messi alitoka nje kipindi cha pili cha mchezo huo, uliopigwa uwanja wao wa nyumbani baada ya kushtua misuli ya mguu, na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu. Enrique amesema kumkosa Messi ni kukosa soka, lakini bado anayo safu ya ushambuliaji iliyo tayari kufanya kazi.
Msanii Barnaba Classic ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa 'lover boy, ametoa sababu inayomfanya asiihusishe sana familia yake kwenye maisha yake ya sanaa, na kusema siyo kitu anachokipa kipaumbele.Barnaba Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Baranaba amesema yeye kama baba wa familia anaijali sana familia yake, na hataki aihusishe na maisha ya sanaa, isispokuwa mashabiki wanachotakiwa kujua ni kazi zake za sanaa tu. "Mimi napenda sana familia yangu, lakini sidhani kama inahitajika kuleta mahusiano yako au familia yako mbele ya hadhara au ya jamii ambayo unaifanyia kazi, sidhani kama maisha yangu ya muziki yanalingana na maisha yangu ya nyumbani, lakini huenda yakawa kichocheo katika sanaa yangu, lakini si kitu ambacho naweza kikawa serious ikawa muda wote watu wanione, hapana" alisema Baranaba. Barnaba aliendelea kwa kusema..... "lakini pia mi ni mtu ambaye nina familia ambayo naitazama tofauti, naipenda familia yangu, napenda wakae kwenye mazingira kama familia, nikirudi nyumbani niwe Elias, nikitoka nje na kwenye kazi yangu naitwa Barnaba, naweka mbali kidogo kumleta mtoto wangu haya mambo, na nina mipango mingi sana na familia yangu lakini sidhani kama jamii inatakiwa ijue zaidi, wao wanachotakiwa wajue ni sanaa yangu na muziki wangu unakwendaje", alisema Barnaba. Barnaba amekuwa mtu wa kuepuka habari za skendo tangu amekuwa baba wa familia, kitu ambacho wasanii wengi hushindwa kuhimili kutenganisha maisha yao ya muziki na maisha binafsi ya familia.
Wednesday, 21 September 2016
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia tiketi ya CCM Hussein Bashe amesema Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama baadhi ya watu wanavyosema bali ni kiongozi mkali anayeshughulikia mambo ambayo yalikuwa yamezoeleka nchini.Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, alipokuwa KIKAANGONi, leo Akizungumza katika kipengele chaKIKAANGONI kinachorushwa LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Bashe ameweka bayana kwamba kwa watu ambao walizoea kupiga dili kwa sasa hivi wamekwama mdiyo maana wanalalamika kuwa ni dikteta. “Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama maana halisi ya dikteta ilivyo , ila ni kiongozi ambaye ni mkali ambaye anapingana na mambo ya kufanya mambo kwa mazoeza 'Business as usual' waliokuwa wamezoea kupiga dili bandarini kwa siku mtu alikuwa anapata laki moja au mbili sasa hiyo imekoma” Amesema Bashe. Aidha kuhusu baadhi ya wananchi kulalamika kwamba pesa hazionekani mtaani, Mbunge Bashe amesema kipindi alipoingia katika uongozi Rais Benjamin Mkapa wananchi walilalamika kwamba pesa zimepotea ila baada ya muda uchumi ukaimarika hivyo kwa sasa wananchi waipe muda serikali ya Rais Dkt John Magufuli. Kuhusu jitihada za kuleta maendeleo Jimboni kake, Bashe ameeleza namna aambavyo ameanza kusaidia vijana ambapo baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kushona wamepelekwa Moshi kujifunza namna ya kutengeneza viatu vya ngozi kwa kuwa jimboni humo anatarajia kujenga kiwanda kidogo cha ngozi. Pamoja na hayo Bashe amewataka wawekezaji ambao wanataka kwenda kuwekeza katika jimbo lake kwenda kwa kuwa watapatiwa ushirikiano wa kutosha na eneo la ardhi tayari lipo.
Rapa aliyekuwa kwenye kundi la Lafamilia, Chiku Keto, amefunguka kuhusiana na sababu ya yeye kulikimbia kundi hilo.Chiku K Akizungumza na eNewz, Chiku K amekanusha kukimbia kundi hilo kutokana na sababu ya kiongozi wao, Chidi Benz, kuathirika na madawa ya kulevya na kusema kuwa kuna sababu nyingine kabisa iliyomfanya akimbie kundini. “Mimi pia nina ndugu zangu ambao pia wameathirika na madawa, tunatakiwa kukemea suala hilo, ni kawaida kwa watu kuzungumzia hilo kusema kamkimbia mchizi sababu alikuwa akitumia madawa ya kulevya siyo vizuri kuzungumza kitu ambacho hukijui. Siri ya mtungi aijuaye kata” Alisema Chiku K. Hataivyo aliweka wazi ujio wake mpya kwenye game la muziki na kuishukuru EATV na EA Radio kwa kuukuza muziki wake na kumuunga mkono.
Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 17 inatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kambi ya siku 10 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville.Mchezo huo utakaopigwa Oktoba 02 ni wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana zitakazofanyika nchini Madagascar mwaka 2017. Kocha wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime amesema, wanaamini mchezo wa marudiano utakuwa na changamoto nyingi lakini wanaamini watajitahidi ili kuhakikisha wanashinda na kuweza kushiriki AFCON hapo mwakani. Shime amesema, anaamini Serikali ya Tanzania ina mkono mrefu hivyo ameiomba kuendelea kutoa sapoti hata timu hiyo itakapokuwa nchini Congo Brazzaville kwa ajili ya mchezo huo ili kuiweka timu ya Serengeti Boys katika hali ya usalama zaidi na kujiona hawapo ugenini. Kwa upande mwingine Shime amewataka watanzania kutokuwa na wasiwasi na timu yao kwani wamejiandaa kushinda kila wakati na wanajitahidi ili kuweza kupata matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano ambayo yatawaweka katika nafasi nzuri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema, hivi sasa wanaendelea na jitihada za kukuza mchezo wa mpira wa magongo nchini.Miongoni mwa mikakati ni pamoja na kushirikiana na Rais wa chama cha mchezo huo duniani FIH pamoja na Rais wa chama cha mchezo huo barani Afrika AFHA ambao wapo nchini kwa ajili ya mikakati ya kuboresha miundombinu na kurudisha heshima ya mchezo huo kama zamani. Nape amesema, mpira wa Magongo (Hockey) ni mchezo ambao ulileta heshima kubwa sana kwa nchi miaka ya nyuma lakini kwa sasa umekuwa haufanyi vizuri katika mshindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi hivyo anaamini ushirikiano huo utasaidia kurudisha hadhi ya mchezo huo nchini. Nape amesema, ameshaongea na Rais wa FIH Leandro Nerge na ameahidi Uwanja ambao utakuwa ukitumika kwa ajili ya mchezo huo na amekiagiza chama cha mchezo wa mpira wa Magongo nchini THA kuandika barua kwa wizara ya michezo ili waweze kuwasiliana na Wizara ya Ardhi ili kuweza kupata eneo zuri litakalojengwa Uwanja. Nape amesema, kwa upande wa Rais wa AFHF Seif Ahmed ameahidi kuongeza miundombinu ya uwanja ikiwa ni pamoja na taa za uwanjani ili kuufanya uwanja kuwa bora zaidi katika matumizi ya mashindano mbalimbali Wakati huohuo Waziri Nape Nnauye ametoa pongezi kwa timu ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens mara baada ya jana kutawazwa kuwa mabingwa wa kwanza kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na kati. Waziri Nape amesema, wameanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu na wataendelea kutoa sapoti kwa timu hiyo ili iweze kuiwakilisha nchi vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali.
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani limesema litafanya ukaguzi kabambe wiki ya usalama barabarani inayotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo magari yatachunguzwa na kuwekewa stika ili kuondoa yaliyo mabovu barabarani.Kaimu kamanda kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu wakati akitoa elimu kwa umma kuhusu usama barabarani, katika kipindi cha SupaMix cha East Africa Radio. “Magari yote yatapimwa na hakuna mtu yeyote ambaye yupo juu ya sheria katika usalama barabarani tutahakikisha vyombo vyote vinapimwa ili ambavyo ni vibovu vikapate matengenezo” Amesema Kamishna Msaidizi Fortunatus. Kwa upnde wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu kwa Umma Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Mossi Ndozero amewataka wananchi kujitokeza kwenye maeneo ambayo yatatangazwa na jeshi la polisi katika mikoa na wilaya kwa ajili ya kupata elimu kuhusu usalama barabarani.
Watu wengine kadhaa wameuawa katika siku ya pili ya machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana, huku makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani yakichomwa moto.Hayo yamejiri katika wimbi jipya la makabiliano kati ya polisi na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila. Machafuko yalizuka upya baada ya Jumatatu ya umwagaji damu ambapo makundi ya upinzani yamesema zaidi ya watu 50 walikufa katika maandamano ya kudai Rais Kabila ajiuzulu. Katibu wa chama kikuu cha upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), Felix Tshisekedi amelilaumu kundi la makomando la utawala kwa kuyachoma makao makuu ya upinzani. Maiti mbili zilizoungua zimeonekana katika afisi za chama hicho. Waandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa, AFP wamesema watu wengine wawili wamechomwa wakiwa hai na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli aliyevuma kitambo, amefunguka na kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnum kurudia moja ya kazi yake anajihisi kuzaliwa upyaSaida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama 'Mapenzi kizunguzungu', Kaisiki, Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000. Saida Karoli amesikika kwenye moja ya clip ambayo ameiposti Diamond Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawamtafuti tena, lakini hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikuwa wakiambiwa kuwa amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imerejesha watu kwenye himaya yake kwani wameanza kumtafuta na kumpigia simu sana. "Mimi nimejisikia vizuri maana hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya mashabiki, mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi tuwe juu kwa hiyo si kazi ya kwangu mimi peke yangu, ila mimi kama mimi nimejisikia vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau leo hii vinanitafuta, haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko duniani wanajua nilishakufa lakini leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya" alisikika Saida Karoli
Tuesday, 20 September 2016
Monday, 19 September 2016
Sunday, 18 September 2016
Katika karne ya 19 lilikuwa jambo la kawaida kwa wazungu kukusanya wanyamapori kutoka sehemu mbali mbali za dunia, na kisha kuwapeleka nyumbani kwao ulaya kuwaweka kwenye makavazi ili waweze kutazamwa. Hata hivyo raia mmoja wa Ufaransa alivuka mipaka zaidi na kupeleka mwili wa mpiganaji mmoja kutoka Afrika. Mwandishi mmoja raia wa uholanzi alikumbana na mwili huo ukiwa kwenye makavazi nchini uhispania miaka 30 iliyopita na tangu wakati huo alikuwa na matumaini ya kufuatila asili ya mtu huyo. Mwili huo ulipata umaarufu kutokana na kusafirishwa kwake na kuwekwa kwa maonyesho ya makavazi kwa kipindi cha miaka 170 nchini Ufaransa na Uhispania.
Paul Mutua, meneja wa bidhaa wa Mamba Village, watalii na wageni mashuhuri wanatarajiwa kufika kushuhudia harusi hiyo. Anasema wanapanga kumwalika waziri wa utalii Najib Balala na hata Rais Uhuru Kenyatta. "Tutakuwa na watalii kutoka humu nchini na tunatarajiwa wageni hata kutoka nje ya nchi," anasema
Subscribe to:
Posts (Atom)